ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa klabu ya Simba, Hamisi Kilomoni, leo Alhamisi Julai 25, 2019, ameachiwa na polisi jijini Dar es Salaam baada ya kukamatwa na kutakiwa kuandika barua ya kuomba ruhusa ya kufanya mkutano na wanahabari.

“Wao wameniambia nimekatazwa, na kwamba lazima nikaombe kibali cha kufanya mkutano,” alisema Kilomoni alipohojiwa na vyombo vya habari.


Kilomoni akipanda gari ya polisi.

Mchezaji huyo wa zamani wa klabu hiyo, alikamatwa na polisi  wakati akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Block 41 Kinondoni,  na kupelekwa katika kituo cha polisi cha Oyster Bay jijini Dar kwa mahojiano