Mwili wa mtu anayeshukiwa kuubiri ndege ya Kenya Airways kisiri ‘stowaway’ umeanguka ndege hiyo ikielekea kutua katika uwanja wa ndege wa Heathrow mjini London.

Kenya Airways”Mtu” huyo alianguka kutoka kwenye ndege ya Kenya Airways iliyokuwa ikisafiri kutoka mjini Nairobi Jumapili mchana

Mwili huo – unaoaminiwa kuwa wa mwanamume – ulipatikana umeanguka katika bustani ya Clapham siku ya Jumapili.

Polisi wanasema mtu huyo alianguka kutoka kwenye ndege ya Kenya Airways iliyokuwa ikisafiri kutoka mjini Nairobi.

Mkoba, maji na vyakula vilipatikana katika eneo lililo chini ya gia ya ndege wakati ilipokua ikutua.

Polisi wa wa jiji la London wamesema mwili huo utafanyiwa uchunguzi kubaini kilichosababisha kifo chake na kwamba kifo chake.

Kenya Airways imesema kuwa ndege hiyo imefanyiwa uchunguzi na hakuna hitilefu yoyote ilioripotiwa.

Msemaji wa shirika la ndege hiyo amesema: “Ndege hii huchukua saa 8 na dakika 50 kukamilisha safari yake. Inasikitisha kuwa mtu alipoteza uhai wake baada ya kuingia ndege yetu kisiri.

“Kenya Airways inashirikiana na mamlaka husika mjini Nairobi na London katika uchunguzi wa tukio hili.”

Sio mara ya kwanza kifo kama hiki kimeripotiwa katika ndege inayoelekea uwanja wa Kimataifa wa Heathrow.

Mwezi Juni mwaka 2015, mtu mmoja alipatikana akiwa amefariki katika paa la makao makuu ya Notonthehighstreet.com katika barabara ya Kew Road, Richmond, huku mwingine akipatikana katika hali mahututi baada ya kuning’inia katika ndege ya British Airways kutoka mjini Johannesburg.

Mwezi Agosti mwaka 2012, mwili wa mwanamume ulipatikana kwenye buti ya ndege iliyokuwa ikitoka mjini Cape Town Afrika Kusini, ilipotua katika uwanja wa Kimataifa wa Heathrow.