Kamanda Jeshi la Polisi mkoa wa kipolisi wa Kinondoni Mussa Taibu amesema ni kweli Jeshi la Polisi linamshikilia Mwandishi Erick Kabendera na yupo anahojiwa ila kuhusu kuachiwa itategemea baada ya kumaliza mahojiano.

Jana katika mitandao mbalimbali ya kijamii zilienea taarifa za nyumba ya mwandishi huyo kuzingirwa nyumbani kwake mbweni na kisha kuchukuliwa.

Kamanda Jeshi la Polisi mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni Mussa Taibu amesema atato taarifa zaidi leo ofisini kwake atakapokuwa na taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo