Mwanaume mmoja ambaye jina lake halikutajwa mwenye umri wa miaka 26, ameomba kupigwa risasi na Polisi wa kituo cha New York Police Department (NYPD), kilichopo Brooklyn jijini New York City.


Mwanaume huyo ambaye inadaiwa kuwa na matatizo ya akili, aliingia katika kituo cha polisi siku ya jana Jumapili saa 2:30 asubuhi, akiwa ameshika kisu na kutaka polisi kumpiga risasi huku akisema kwa lugha ya Kihispania kuwa "Serikali inanizingua tu, Mimi nataka mnipige risasi".

Baada ya kusema hivyo polisi walimuamuru kushusha kisu chake chini lakini Mwananume huyo alikataa na kuendelea kuhoji kwanini hawampigi risasi.

Polisi wa kituo hicho waliamua kumpiga risasi ya mguu na kwasasa yupo hospital akipatiwa matibabu ya majeraha aliyoyapata na polisi wamesema watalifanyia uchunguzi tukio hilo.