Mwalimu wa Shule ya Msingi Rung’abure Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Godfrey Tarimo (35) amenusurika kifo baada ya kujikata shingo kwa chupa, huku sababu ikidaiwa kuwa ni ugumu wa maisha.

Akizungumza na Gazeti la Mwananchi jana Julai 4, 2019 Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu amesema tukio hilo limetokea jana Jumatano Julai 3, 2019.

Mwalimu huyo amelazwa katika hospitali teule ya Nyerere wilayani humo anakoendelea na matibabu.

Mganga mkuu wa hospitali hiyo,Tanu Warioba amesema kuwa Tarimo alifikishwa hospitalini hapo akiwa anavuja damu katika jeraha hilo.

Datar amesisitiza kuwa mgonjwa hakupata athari yoyote katika mfumo wake wa upumuaji.

Amesema maelezo waliyoyapata awali ni kuwa mwalimu huyo alichukua hatua hiyo kwa madai ya ugumu wa maisha, kwamba baada ya kupatiwa matibabu ameanza kuzungumza kwa tabu.