Timu ya wafanyakazi wa Benki ya Standard Chartered wametandikwa goli moja kwa bila na timu ya Wanahabari katika mechi ya uzinduzi wa kombe la Standard Chartered.

Mchezo huo wa dakika 10 mpaka wanaenda mapumzikoni walikuwa suluhu ya kutofungana. Lakini dakika ya pili ya kipindi cha pili Mwandishi wa Habari za Michezo wa ITV Sebastian Kolowa alitungua goli la benki ya Standard Chartered na kufanya mpira huo kumalizika kwa goli 1-0.

Ufunguzi huo wa michuano ya Kombe la Standard Chartered Bank wakishirikiana na timu ya Liverpool ya Uingereza umefungua msimu wa nne mfululizo kufanyika nchini Tanzania.

Akizungumza katika ufunguzi huo Kaimu Mkurugenzi wa Standard Chartered Bank Tanzania, Rayson Foya amesema kwamba michuano hiyo itakuwa na timu 32 za kampuni mbalimbali zenye wachezaji saba. Alisema kwa sasa dirisha lipo wazi la usajili mpaka Agosti 16 kabla ya michuano hiyo kuanza kuunguruma rasmi Agosti 24, mwaka huu.

Michuano hiyo itafanyika katika Uwanja wa JMK Park, Dar es Salaam na mfumo utakaotumika wa mechi hizo ni kila timu kuingia uwanjani na wachezaji watano wakiwa na wachezaji wa akiba wawili. Kila mechi itachezwa kwa dakika 10.

Timu itakayoibuka bingwa itapata nafasi ya kwenda katika Uwanja wa Anfield, England unaotumiwa na Liverpool na kupata nafasi ya kukutana na wakongwe wa timu hiyo na kupata nafasi ya kushuhudia moja ya mechi za Liverpool kwenye michuano ya Ligi Kuu England.

Alisema kwamba michuano hiyo itafanyika kwa Knock outs.
Benki ya Standard itagharamia safari za wachezaji saba wa timu itakayoshinda yaani tiketi za ndege na malazi yao kwa siku tatu.
Aidha alisema mwaka huu hawatawaleta magwiji wa nje na badala yake watatumia magwiji wa hapa nyumbani kuhakikisha soka linaendelezwa.

 “Pamoja na yote hayo lakini safari hii Standard Chartered tumeamua kushirikiana na TFF (Shirikisho la Soka Tanzania) na wakongwe wa soka nchini kwa ajili ya kupanua wigo wa vipaji na kukuza soka nchini kote. Kwa hiyo kwa kuanza tutakuwa na Ali Mayay na wengine ambao tutakuwa nao wakati wa michuano hii,” alisema Foya.

Kipindi kilichopita Benki hiyo iliwaleta magwiji wa soka wa Liverpool akiwemo Sami Hyppia huku mwaka juzi walimleta John Barnes kwa lengo la kukuza vipaji.
Kuwapo kwa kombe hilo ni matokeo ya udhamini wa benki ya The Standard Chartered Group kuanzia mwaka 2010. Na mwaka jana ilitia saini ya kuendelea na udhamini hadi msimu wa mwaka 2022/23.

Kombe hilo ni sehemu ya makubaliano kati ya beniki hiyo na klabu ya Liverpool ya kuendeleza mahusiano yake na nchi ambazo inafanya nazo biashara  Asia, Africa na mashariki ya Kati, kwa lengo la kuinua soka. Mashindano hayo kwa sasa yapo katika mwaka wa nane na yanazidi kuwa na nguvu yakianzia Singapore mwaka 2012.
 Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba (kushoto) akitambulisha meza kuu kwa waandishi wa habari Kutoka kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Standard Chartered Bank Tanzania, Bw. Rayson Foya, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bw. Wilfred Kidau, Mchambuzi mkongwe wa soka nchini ambaye ni shabiki wa timu ya Liverpool, Dk. Leaky Abdallah pamoja na Mkongwe wa soka nchini, Bw. Ali Mayay wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kombe la Standard Chartered Bank uliofanyika katika viwanja vya JMK Park jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi wa Standard Chartered Bank Tanzania, Bw. Rayson Foya (wa pili kushoto) akizungumza kuhusu mashindano ya kombe la Standard Chartered Bank ambapo dirisha la usaji wa timu limefunguliwa rasmi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kombe hilo uliofanyika katika viwanja vya JMK Park jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba na wa tatu kushoto ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bw. Wilfred Kidau pamoja na Mchambuzi mkongwe wa soka nchini ambaye ni shabiki wa timu ya Liverpool, Dk. Leaky Abdallah
 Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bw. Wilfred Kidau (katikati) akizungumzia mipango ya TFF kwa kushirikiana na Benki ya Standard Chartered katika kuinua soka la Tanzania kupitia michuano ya kombe la Standard Chartered Bank wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mashindano ya kombe hilo uliofanyika kwenye viwanja vya JMK Park jijini Dar.
 Mchambuzi mkongwe wa soka nchini ambaye ni shabiki wa timu ya Liverpool, Dk. Leaky Abdallah (wa pili kulia) akitoa tathmini ya timu ya Liverpool kuelekea michuano ya Ligi Kuu England wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kombe la Standard Chartered Bank uliofanyika katika viwanja vya JMK Park jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkongwe wa soka nchini, Bw. Ali Mayay na kutoka kushoto ni Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba, Kaimu Mkurugenzi wa Standard Chartered Bank Tanzania, Bw. Rayson Foya pamoja na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bw. Wilfred Kidau.
 Mkongwe wa soka nchini, Bw. Ali Mayay  (kulia) akielezea furaha yake kushiriki kwenye mashindano ya kombe la Standard Chartered Bank yatakayoanza kutimua vumbi mwezi ujao wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kombe hilo iliyofanyika katika viwanja vya JMK Park jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba akisalimiana na kikosi cha wanahabari wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kombe la Standard Chartered Bank uliofanyika katika viwanja vya JMK Park jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bw. Wilfred Kidau na Kaimu Mkurugenzi wa Standard Chartered Bank Tanzania, Bw. Rayson Foya wakisalimiana na timu ya wanahabari  iliyochuana na wafanyakazi wa benki ya Standard Chartered wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kombe la Standard Chartered Bank uliofanyika katika viwanja vya JMK Park jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi wa Standard Chartered Bank Tanzania, Bw. Rayson Foya, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bw. Wilfred Kidau, Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba, Mchambuzi mkongwe wa soka nchini ambaye ni shabiki wa timu ya Liverpool, Dk. Leaky Abdallah pamoja na Mkongwe wa soka nchini, Bw. Ali Mayay  wakiwa kwenye picha ya pamoja na timu ya wafanyakazi wa benki ya Standard Chartered pamoja na timu ya wanahabari walioshiriki hafla ya uzinduzi wa kombe la Standard Chartered Bank uliofanyika katika viwanja vya JMK Park jijini Dar es Salaam. Timu ya wafanyakazi wa Benki ya Standard Chartered (jezi nyekundu) na timu ya wanahabari (jezi nyeusi) wakimenyana kuashiria uzinduzi wa kombe la Standard Chartered Bank 2019 katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja vya JMK Park jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi wa Standard Chartered Bank Tanzania, Bw. Rayson Foya, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bw. Wilfred Kidau pamoja na Mkongwe wa soka nchini, Bw. Ali Mayay wakiwa kwenye picha ya pamoja na timu ya wanahabari iliyoibuka kidedea kwa goli 1-0 dhidi ya timu ya wafanyakazi wa benki ya Standard Chartered wakati wa hafla ya uzinduzi wa kombe la Standard Chartered Bank uliofanyika katika viwanja vya JMK Park jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bw. Wilfred Kidau akitoa zawadi kwa timu ya wanahabari iliyoibuka kidedea kwa goli 1-0 dhidi ya timu ya wafanyakazi wa benki ya Standard Chartered wakati wa hafla ya uzinduzi wa kombe la Standard Chartered Bank uliofanyika katika viwanja vya JMK Park jijini Dar es Salaam.