Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini Marc Batchelor amepigwa risasi na kufariki

Picha za eneo la tukio zinaonyesha risasi zilipita kwenye dirisha la kioo cha gari lake na waliofanya tukio hilo inaelezwa walikuwa wamepanda pikipiki.

Batchelor atakumbukwa sababu ni miongoni mwa wachezaji wachache waliocheza timu hasimu nchini Afrika kusini, Kaizer Chiefs na Orlando Pirates.