Msanii wa muziki nchini Marekani, R Kelly amekamatwa na Idara ya Polisi ya New York kwa tuhuma za kuwasafirisha wanawake kwa ajili ya kuwatumikisha kingono. Muimbaji huyo amekamatwa wakati akiwa katika Jimbo la Chicago

Mwanamuziki huyo wa miondoko ya R&B anatuhumiwa kwa makosa 13 yanayohusisha ukatili wa kingono dhidi ya Watoto

Hii ni mara ya 3 kwa R. Kelly kukamatwa, alikamatwa mara ya kwanza mwezi Februari kwa tuhuma za kuhusika na makosa 10 ya ngono

Mwezi Mei alikamatwa tena na kushtakiwa kwa tuhuma za kuhusika na makosa 11 ya unyanyasaji wa kingono ambapo kati ya makosa hayo yalikuwemo yanayohusisha kifungo cha hadi miaka 30 jela