Mpenzi wa Diamond Platnumz, Tanasha azungumzia ujauzito wake
Mpenzi wa mwanamuziki Diamond Platnumz, Tanasha Dona ameeleza ni kwa jinsi gani alivyokuwa na furaha pia atoa shukurani kwa kuweza kupata baraka ya mtoto huku akikazia kumlinda na mambo mabaya.

Kwa mujibu wa Tanasha, hapo mwanzo alihisi hayuko tayari kuwa mama lakini kadri siku zilizozidi kwenda alipata kuelewa na kufurahia hali hiyo.

Pia Tanasha amemsifia mwanae huyo na kudai kuwa ni 'Handsome' baada ya kuangalia picha za 3D UltraSound. Ameeleza hayo yote kupitia ujumbe aliochapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram.