Sanamu ya jiwe ya miaka 3000 ya Farao wa Misri, Tutankhamun imeuzwa kwa mnada kwenye jumba la mnada la Christie's mjini London kwa kiasi sawa na Euro milioni 5.3.
Wizara ya mambo ya nje ya Misri mjini Cairo tayari imeeleza kukasirishwa na mnada huo, ambao umefanyika kinyume cha makubaliano na mikataba ya kimataifa.
Waziri wa zamani wa mambo ya kale wa Misri, Sahi Hawass, amesema sanamu hiyo yumkini iliibwa kutoka jengo la hekalu katika miaka ya 1970.
Hawass alipigania kurejeshwa kwa hazina za kale za utamaduni wa Misri kutoka ng'ambo. Sanamu hiyo imenunuliwa na mzambuni ambaye hakutajwa jina.