MSANII anaye-fanya vizuri na ngoma yake ya Mua, Mariene Mdee ‘Mimi Mars’ amefunguka kufuata nyayo za dada yake Vanessa Mdee ‘Vee Money’ ili aweze kufika mbali kimuziki kwa sababu ana ndoto kubwa za kuwa mwanamuziki wa kimataifa.

Akipiga stori na Showbiz, Mimi Mars alisema Vanessa ni msichana anayejituma vilivyo kwenye kazi yake na malengo yake makubwa ni kufika mbali kimuziki hivyo kupitia dada yake huyo anaamini ipo siku at afikia levo hizo za juu zaidi.

“Unajua Vanessa ni dada yangu hivyo naona juhudi anazozitumia katika kuufikisha muziki wake mbali zaidi, anajituma sana, hapati hata muda mzuri wa kupumzika na ndiyo maana hata akigombana na mpenzi wake hawazi sana kwa sababu muda mwingi yupo bize, kiukweli nafuata nyayo zake na natamani siku moja na mimi niweze kuufikisha muziki wangu kimataifa zaidi,” alisema Mimi Mars