Shule ya Sekondari ya Kigonsera iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma ambayo ilianzishwa mwaka 1938 ikiwa na Historia kubwa ya kusomesha viongozi wengi wa kitaifa akiwemo Rais wa awamu ya tatu. Mh. Benjamin Mkapa na Waziri Mkuu wa sasa, Mh. Kassim Majaliwa imeanza kufanyiwa ukarabati mkubwa baada ya Rais John Pombe Magufuli kutoa kiasi chaA fedha milioni 931 kwa ajili ya ukarabati mkubwa katika shule hiyo.