Wachezaji nyota wa Arsenal Mesut Ozil na Sead Kolasinac wameripotiwa kuvamiwa na genge la majambazi katika jaribio la wizi wa gari katika barabara za mji wa London.
Klabu ya Arsenal imethibitisha kuwa wachezaji wake Mesut Ozil na Sead Kolasinac walilengwa na majambazi hao waliokua wamejihami lakini hawakujeruhiwa katika tukio hilo.
Ozil and KolasinacHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionSead Kolasinac na Mesut Ozil
Kanda ya video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii inamuonesha Kolasinac akipigana na na wanaume wawili waliokuwa wamejihami kwa visu.
Mchezaji huyo pia anaonekana akiruka kutoka kutoka kwenye gari kukabiliana na wanaume waliokuwa wameficha nyuso zao na ambao walikuwa na njama ya kuwaibia.
Msemaji wa polisi wa jiji la London amesema: “Tumepata taarifa kuwa washukiwa waliokuwa juu ya pikipiki walijaribu kumuibua mtu aliyekuwa akiendesha gari.
“Dereva pamoja na abiria wake walifanikiwa kuondoka eneo la tukio bila kujeruhiwa na kwenda hadi eneo la Golders Green, ambako wamewasilisha taarifa kwa maafisa wetu.”
Kolasinac na Ozil ni wachezaji wa kwanza wa soka kuvamiwa katika barabra za London.
Mwaka 2016, aliyekuwa wakati huo mshambuliaji wathen West Ham Andy Carroll alitishiwa kwa bunduki alipokuwa njiani kwenda nyumbani kutoka mazoezini.
Baada ya tukio hilo Kolasinac ameandika ujumbe huu kwenye ukurasa wake wa Twitter,