Mchezaji kutokea Brazil, Gerson Vieira amesema maisha mapya ndani ya kikosi cha Simba SC ni yenye kumfurahisha zaidi.

Ameeleza hayo nchini kambini mjini Rusterburg, Afrika Kusini ambapo Simba SC wapo kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi.

“Ninafuraha sana kuwa hapa, wachezaji wenzangu walinipokea na kila mmoja yupo vizuri, na tuna kocha mwenye uwezo mkubwa. Najivunia sana kuwa sehemu ya familia hii.” amesema Gerson Vieira.

Ligi ya Mabingwa Afrika Simba SC itaanza kwa kumenyana UD do Songo ya Msumbiji katika Raundi ya kwanza. Mabingwa hao wa Tanzania Bara wataanzia ugenini kati ya Agosti 9 na 11 kabla ya kurejea nyumbani kwa mchezo wa marudiano kati ya Agosti 23 na 25.