Mchezaji raia wa Brazil, Alessandro ameshindwa kujiunga na timu yake mpya ya Daejeon Citizen ya Korea baada ya kupatikana na virusi vya UKIMWI alipofanyiwa vipimo vya afya.


Mchezaji huyo alikamilisha hatua zote za kujiunga na klabu hiyo na kilichokuwa kikisubiriwa ni vipimo vya afya ili asaini mkataba mpya.

Lakini baada ya kupatikana na dosari hiyo, klabu iliamua kukatisha mkataba na mchezaji huku msemaji wa klabu akisema, "hatutoruhusu kitu kama hiki kutokea tena" na kuelezea kuwa klabu imepanga kusajili wachezaji watatu.

Klabu ya Daejeon Citizen imekuwa nje ya kiwango bora katika ligi kuu ya nchini Korea tangu mwaka 2016, ambapo msimu uliopita iliishia kumaliza nafasi ya pili kutoka mkiani