MLINZI wa spika wa bunge la kaunti ya Meru, Joseph Kaberia, ameuawa kwa kupigwa risasi jijini Nairobi nchini Kenya.

Vyombo vya habari nchini Kenya vimeripoti kuwa mlinzi huyo alipigwa risasi jana Jumapili, Julai 21, katika eneo la Kamiti Corner.

Kwa mujibu wa polisi, nchini humo wanasema mlinzi huyo alikuwa  na dereva wa spika wakati tukioh ilo linatokea.

Dereva huyo amekamatwa ili kusaidia polisi katika uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo huku polisi wakishuku pia huenda alihusika kwa njia fulani.

Polisi walifika katika eneo la tukio hilo ambapo waliwakuta wawili hao huku mlinzi akiwa amepigwa risasi kifuani na dereva kwenye mguu  na wote  walikimbizwa hospitalini ambapo mlinzi huyo alifariki akiwa anapokea matibabu.