Msanii nguli wa muziki wa Bongo Fleva, Matonya amefunguka suala lake la kumiliki nyumba za kifahari ndani na nje ya Tanzania.
Amesema hayo kupitia EATV/Radio Digital, baada ya kuulizwa endapo ana mpango wowote wa kumiliki nyumba au makazi yake, ambapo amesema anamiliki nyumba Jijini Dar Es Salaam, Tanga na Nairobi.
“Tulifanikiwa kufanya hivyo vitu lakini sasa hivi tuna mipango mingine tofauti, masuala ya ujenzi tulishafanikiwa muda mrefu namshukuru Mwenyezi Mungu, Tulijenga mijengo mingi sio Tanga tu ukifika Dar es Salaam na Nairobi na sehemu zingine tofauti kwenye hiyo hatua tulishavuka”, amesema Matonya.
Matonya ameongeza kusema kuwa anaendelea na mipango yake mingine ya kufanya biashara zake binafsi na kazi za kimuziki ambayo ndiyo imemtoa kimaisha mpaka sasa.
Pia msanii huyo anajivunia kutoa mchango wake wa kumsaidia msanii Marioo, ambaye amepitia mikononi mwake na sasa anafanya vizuri vizuri sana kwenye soko la muziki wa Bongo Fleva hapa nchini Tanzania