Staa na mwimbaji maarufu kutokea Nigeria Burna Boy akiwa mbioni kuiachia Album yake ya nne  “African Giant “ inayotajwa kuachiwa rasmi July 26,2019 ameachia rasmi ngoma zitakazopatikana kwenye album yake pamoja na wasanii aliowashirikisha.

Album hiyo ya ‘African Giant’ itajumuisha jumla ya ngoma 19 ikiwa na nyingine ambazo aliwahi kuziachia mfano The Low, Dangote, Gbona na Anybody, Burna Boy amewashirikisha wakali kibao akiwemo YG(Marekani), Damian Marley (Jamaica) , Angelique Kidjo(Marekani), Future(Marekani), Jorah Smith(Marekani), Jeremih, Jorja Smith na wengine kibao  ambao watasikika kwenye album hiyo.Album hiyo itakua ni ya nne ambapo album yake ya tatu ‘Outside” aliiachia January 26, 2018 ikiwa album hiyo ilijuisha midundo ya Afro Pop, Rap pamoja na dancehall ilihusisha sauti za wakali kutokea Uingereza kama J Hus, Lilly Allen and Mabel