Mkufunzi kutoka Kampuni ya Mantrac, Ehab Abdelfatah Mohamed, (mwenye miwani) akitoa maelezo kwa baadhi ya waendeshaji kutoka makampuni tofauti  kuhusu mashine mpya za uchimbaji aina ya Caterpillar,  zinazosambazwa na kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Waendeshaji hao wanahudhuria mafunzo ya siku tatu yaiyoandaliwa na kampuni ya Mantrac Tanzania. 
Mmoja wa washindi wa shindano lililoandaliwa na Mantrac Tanzania lijulikanalo kama ‘The Operator Challenge’ ikiwa ni sehemu ya mafunzo ya siku tatu kwa waendeshaji wa makatapila, Samwel Leonard (kushoto) akipokea zawadi yake kutoka kwa Mkufunzi kutoka Kampuni ya Mantrac, Ehab Abdelfatah Mohamed.

Kampuni ya Mantrac, ambayo ina idhini ya kuingiza nchini mashine za uchimbaji maarufu kama caterpillar, imewazawadia wateja wake kwa namna ya kipekee kwa kutoa mafunzo kwa wateja wake ili waweze kuelewa namna ya kuendesha mashine zao mpya.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Meneja Mauzo wa Mantrac Tanzania, Butwa Sanga, alisema mafunzo hayo ya siku tatu yaliyojulikana kama ‘The Operator Challenge’, yaliandaliwa mahususi kwa waendeshaji hao ili kuwaongezea ujuzi hasa wanapotumia mashine mpya zinazojulikana kama New Generation Hydraulic Excavator (NGH).
Alisema mashine hiyo mpya ya NGH inalenga kuongeza ufanisi wa hali ya juu, kupunguza gharama na kupunguza muda wa kufanya kazi na hivi kuongeza uzalishaji.
“Makatapila haya mapya ya NHG yanapunguza muda wa kazi kwa nusu na wakati huo huo kupunguza matumizi ya mafuta kwa kati ya asilimia 25 na kuongeza ufanisi kwa hadi asilimia 45,” alisema.
Alisema mafunzo hayo ya siku tatu yalidhaminiwa na Mantrac Tanzania na kuendeshwa na mtaalamu wa mafunzo Ehab Abdelfatah Mohamed kutoka Misri.
“Tunataka waendeshaji hawa wapate ujuzi zaidi kuhusu makatapila haya mapya kwani yana teknolojia ya juu zaidi ukilinganisha na mengine ya nyuma,” alisema na kuongeza kuwa uzinduzi rasmi wa katapila hiyo mpya ya NHG utafanyika Julai 17 mwaka huu Jijini Dar es Salaam.
Mafunzo hayo pia yalienda pamoja na zoezi maalumu lijulikanalo kama ‘The Operator Challenge’ ambapo waliofanya vizuri zaidi walipokea zawadi na vyeti.
Mmoja wa wahudhuriaji wa mafunzo hayo, Samuel Leonard, ambaye alipokea moja ya tuzo za juu  alisema mafunzo hayo yalikuwa muhimu katika kuhakikisha wanaweza kuendesha mashine hizo mpya bila matatizo.
“Tunajifunza kila siku na hasa ukizingatia makatapila haya mapya yana teknolojia ya juu sana, mafunzo haya ni muhimu sana kwetu,” alisema.