MAMA wa msanii nyota wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul, maarufu kama Diamond Platinumz, anayefahamika kwa jina la Bi Sandra (Sandura Kassim) amekanusha tetesi za mwanaye kudaiwa kutumia madawa ya kulevya.

Mama huyo amesema mwanaye amekuwa akifanya kazi sana kila kukicha hivyo anachoka sana na si kweli kwamba anatumia madawa kwani Diamond anajua fika madhara ya kutumia madawa na kama angetaka kutumia basi angeanza zamani alipokuwa akiishi Tandale.