VIDEO vixen ambaye kwa sasa amejiingiza kwenye Muziki wa Bongo Fleva, Irene Louse ‘Lynn’ amekiri kutoka maisha ya uswahilini na kutoboa kimaisha.


Akistorisha na Za Motomoto, Lynn ambaye kwa muda mrefu amekuwa akijionesha maisha ya kishua alisema kuwa, wasichana wengi wanakata tamaa ya maisha waliyopitia kumbe ndio yangewafanya wasimame.


“Kujiamini tu jamani, kuna wengine wanadharau sana wasichana wanaoishi maisha ya uswahili yaani kule ndio naamini kabisa kuna wasichana wa ukweli kikubwa ni kujiamini. Mimi ni mtoto Buguruni tena uswahilini tu lakini ngumu kuamini ni vile tu nilivyojitengeneza hadi kuwa hivi nilivyo,” alisema Lynn.