Video vixen ambaye huko nyuma alibeba skendo ya kutoka kimapenzi na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Irene Loius ‘Lynn’ amerusha dongo ambalo limetafsiriwa kuwa amemlenga mpenzi mpya wa jamaa huyo, Tanasha Donna. Lynn alikaririwa akisema yeye ana magari manne, lakinihana mimba hivyo watukujiongeza na kudai alimlenga Tanasha ambaye kwa sasa ana mimba ya Diamond. Lynn aliliambia Gazeti la Ijumaa Wikienda kuwa, hajawahi kumtaja Tanasha kwenye mambo yake, bali alijisemea tu anamiliki magari manne na bado hana ujauzito.
“Nilijisemea tu na sikuwa ninamaanisha kumsema mtu yeyote. Kwani kuna kosa kusema nina magari manne na sina mimba jamani?” Alihoji Lynn aliyeuza sura kwenye Video ya Kwetu ya Rayvanny.