MBUNGE wa Jimbo la Mtera (CCM), Livingstone Lusinde leo Julai 20, 2019 amekiongea na wanahabari  katika Hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salam amemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola kutowaita Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kuwaita na kuwahoji kufuatia sauti inayosambaa mitandaoni ikidaiwa ni yao.

Akiongea na wanagabari leo

”Kwenye chama chetu hakuna mgogoro; ndani ya Chama Cha Mapinduzi kuna watu  wawili-watatu wanalumbana nao ni makatibu wakuu wa CCM na Musiba, sasa huo huwezi kumaanisha ni mgogoro ndani ya CCM.””Musiba akizungumza wale wazee walikuwa wakimsikiliza tuhuma anazowapa. mwishoni wao wakaamua watoe waraka wa kumjibu Musiba.  Ule waraka haukumjibu Musiba tu, umeenda mbali zaidi.”

”Nataka niseme kuwa wazee wangu wamepotoka kwa kutoa waraka ambao umewaonyesha ni wanasiasa wazoefu, lakini Musiba amewaendea kwenye jicho wasiloliona, hawakupaswa kutoa huo waraka.””Walitakiwa watafute kijana wa kumjibu Musiba, au wao wenyewe watafute press wamjibu Musiba siyo kuandika waraka utakaobaki maishani mwao kwamba viongozi wa kisiasa wa ngazi za juu Kinana na Makamba wanaandika kumlalamikia Musiba ni vitu ambavyo naona vimewafedhehesha sana.”

”Jambo la pili ambao nataka nilizungumzie hapa ni ‘klip’ ambayo inasambaa, ukiisikiliza ni sauti ya Katibu Mkuu Mstaafu Kinana na Nape.  Ukisikiliza kuna maneno ya fedheha kwa mkuu wa nchi.”

“Bernard Membe namweka kiporo, naenda safari China kwa ziara ya kazi za kibunge, nikirudi nitamshughulikia.  Nitamkuna panapomwasha. Membe hana lolote.”

“Mwenyekiti wetu ikimpendeza, ile taarifa ya Dk. Bashiru inayohusu wizi wa mali za CCM irushwe kwenye vyombo vya habari, ili wananchi wajue, walioiba mali za CCM.”“Nina uhakika Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally amesikia lakini namshangaa Lugola amekaa kimya, haiwezekani wengine wafungwa kwa kumtukana Rais, hawa watu inabidi wahojiwe walikuwa na maana gani.”“Mimi nafurahi Musiba kutukana viongozi wastaafu, sababu Kinana alitukana viongozi wake akawaita mizigo, Nape amepata umashuhuli kwa ajili ya matusi, nashangaa wanakasirika nin, wakati wameuunda utaratibu huu.”“Hakuna Mbunge anayepangwa, mimi sihitaji kutumwa na mtu, najituma mwenyewe, mimi sijaja kumtetea Musiba, kazi aliyoifanya Musiba ilikuwa inafanywa na Nape kwa hiyo wasilalamike hiyo kazi walishaianza wao.”“Hakuna Mbunge anayepangwa, mimi sihitaji kutumwa na mtu, najituma mwenyewe, mimi sijaja kumtetea Musiba, kazi aliyoifanya Musiba ilikuwa inafanywa na Nape kwa hiyo wasilalamike hiyo kazi walishaianza wao.”“Kinana na Mzee Makamba wana nafasi ya kuzungumza na Rais John Magufuli, hawakuitumia hiyo wakaamua kuandika waraka. Haina maana.”