MWANAMUZIKI mrembo anayekuja juu kwa kasi kwenye bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ ameweka wazi mapenzi yake motomoto na mwanamuziki wa Kenya, Charles Kanyi almaarufu Jaguar.Lulu Diva aliliambia Gazeti la Ijumaa Wikienda kuwa, yeye na jamaa huyo, wikiendi iliyopita walikuwa wanakula bata la hatari huko Dubai.


Lulu Abbas ‘Lulu Diva’.

Tukio hilo lilikuja baada ya Jaguar ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Starehe nchini Kenya kuomba Watanzania radhi kufuatia matamshi yake ya mwezi uliopita kwamba waondoke nchini Kenya.

Katika mahojiano na Gazeti la Ijumaa Wikienda kwa njia ya simu, Lulu alisema ameamua kuanzisha penzi jipya na Jaguar, akiamini labda akijaribu penzi nje ya Tanzania anaweza kudumu kwa muda mrefu tofauti na uhusiano wake mwingine aliopitia.Ijumaa Wikienda: Umesema upo Dubai unakula bata na Jaguar, mbona uhusiano huu kama umekuja ghafla sana?


Lulu Diva: Wala siyo ghafla kama watu wanavyodhani. Tulianza kama miezi minne nyuma na sasa tumeamua kuweka wazi.Ijumaa Wikienda: Mbona inasemekana Jaguar amekuja kumuona mtoto wake Tanzania?Lulu Diva: Mimi hayo siyajui kabisa, ninachoangalia ni penzi langu mimi. ijumaa Wikienda: Sasa hukujisikia vibaya kutoka na mtu ambaye alitangaza kuwafukuza Watanzania nchini kwao?Lulu Diva: Mimi niko kwenye mapenzi, hayo mengine hayahusiani na penzi langu. ijumaa Wikienda: Kwa hiyo Dubai mnafanya nini?Lulu Diva: Ni kula bata tu, baadaye tutakwenda zetu Nairobi nyumbani kwa wakwe. ijumaa Wikienda: Haya endeleeni kufurahia.Lulu Diva: Asante sana, nawe tunakukaribisha. Kabla ya penzi hilo jipya, Lulu Diva aliwahi kudaiwa kutoka kimapenzi na watu kadhaa akiwemo mwanamuziki wa Bongo Fleva, Richard Martin ‘Rich Mavoko’ aliyefanya naye Wimbo wa Ona.