Mamlaka ya hali ya hewa nchini TMA, imesema usiku wa Julai 17, kutatokea hali ya kupatwa kwa mwezi, ambapo tukio hilo hujirudia mara chache sana katika maeneo husika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo, imeeleza kuwa tukio hilo ni la kupatwa kwa mwezi sehemu (Penumbra), ambalo litaonekana katika nusu ya Dunia, hususani maeneo ambayo tarehe hiyo itakuwa usiku, ikiwemo Ulaya, Asia, Australia na Afrika.

Kwa hapa nchini  hali hiyo inatarajiwa kuonekana majira ya saa 3 hadi saa 9 usiku.

Aidha imeelezwa kuwa tukio hilo halina athari yoyote, ila upo uwezekano wa kuongezeka kwa kina cha maji katika bahari na kwamba hali hiyo inaelezwa kusababishwa na mvutano  kati ya mwezi na maji katika bahari.