Kocha Mkuu wa Simba SC, Patrick Aussems amefunguka mara  baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Orlando Pirates kumalizika kwa sare ya kufungana goli 1-1.

Aussems amesema ameridhika kwa namna timu yake ilivyocheza mchezo huo na kambi waliyoweka nchini Afrika Kusini imekuwa yenye mafanikio sana.

“Tumemaliza kambi na Orlando Pirates ambao wapo tayari kuliko sisi [muda walitumia kujiandaa na msimu mpya] lakini tumecheza vizuri. Napenda kuwapongeza wachezaji wangu tulikuwa na wakati mzuri sana Rustenburg, kila mmoja kafanya kazi nzuri tunaweza kusema hii kambi imekuwa nzuri sana na nimeridhishwa” amesema Kocha huyu.

Huo ulikuwa mchezo wa nne wa kujipima nguvu kwa Simba SC katika kambi yake ya Afrika Kusini kujiandaa na msimu mpya, baada ya awali kushinda mechi mbili mfululizo na kutoa sare moja.
HABARI HIZI ZOTE UTAZIPATA KATIKA APP YETU YA MUUNGWANA BLOG  BOFYA HAPA KU-DOWNLOAD SASA .