Kwa takribani wiki moja sasa kumekuwa na picha za watu  kwenye mitandao ya kijamii zikiwaonesha sura zao za uzeeni, Jambo ambalo limewavutia sio tu watu wa kawaida bali hata watu maarufu duniani wamekuwa wakiposti picha hizo kwa kutumia programu ya Face App.Sasa kufuatia ongezeko la watumiaji wa App hiyo, Seneta Mwandamizi wa jiji la New York nchini Marekani, Chuck Schumer amewataka watumiaji wa App hiyo kuwa makini kwani huenda data zao za utambuzi wa sura zikadukuliwa.

Schumer akitoa tahadhari hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter, Amewata FBI kufanya uchunguzi kuhusu App hiyo ambayo imekuwa ikitumika kubadili picha ya mtu kumuonyesha akiwa mzee.

Hata hivyo, Tayari tuhuma hizo za Schumer, zimejibiwa na kampuni ya Wireless Lab ambayo ndiyo wamiliki wa App hiyo. Ambapo wamesema japokuwa makao makuu ya app hiyo yapo Urusi ila Servers zinazotumika katika kupokea na kuhariri picha mpya hazipo nchini Urusi.

FaceApp nimejipatia umaarufu kwa muda mfupi duniani, Ambapo Marekani yenyewe inatajwa kuwa moja ya nchi yenye watumiaji wengi wa App hiyo.