Mvulana mmoja mwenye umri wa miaka 13 kutoka kwa familia masikini aliyepenyeza ndani ya uzio wa uwanja wa ndege wa Huzhou nchini China na kuendesha ndege mbili bila kibali.

Hata hivyo, amepigwa na butwaa kufuatia adhabu ya kipekee aliyetozwa baada ya kugongesha ndege moja kwenye uzio wa uwanja huo.


Wakuu wa uwanja huo waliamua kuipunguzia familia yake faini ya dola 1,162 ilimradi atajiunga na chuo cha urubani.

Mkurugenzi mkuu wa uwanja huo amenukuliwa akisema ''Ni vigumu sana kuendesha ndege bila mafunzo wala uzoefu, huyu lazima ni kijana mwerevu mno''.