Na Blasio Kachuchu, Dodoma.

Jeshi la polisi Mkoani Dodoma linamshikilia Kijana mmoja Donald Justine (25) baada ya kumvizia na kumbaka bibi kizee mwenye umri wa miaka 95 huku yakitajwa Matukio ya ukatili kuongezeka kutoka 174 mwaka 2018 hadi matukio 517 mwaka 2019 mkoani humo.

Akizungumza na waandishi wa Habari Julai 4,2019, Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, Kamishna msaidizi wa polisi, Gilles Muroto (pichani) amesema Katika eneo la Nane nane kata ya Nzuguni, Dodoma Mjini, kikongwe wa miaka 95, mkazi wa eneo hilo alibakwa na kijana mmoja Donald Justine (25) aliyemvizia akiwa amelala na kumkaba shingoni kisha kumtendea unyama huo.

Kamanda Muroto ameyataja matukio mengine ,Katika kijiji cha Mlazo, tarafa ya Mpyayungu, Wilaya ya Chamwino, Makame Wambura, (28) na mtoto wake Fidelika Walioba miezi mitatu(3) baada ya kumwagiwa mafuta ya petrol na mume wake aitwae Elias Warioba (30) na wote wawili kujeruhiwa vibaya na wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma, na hapa kamanda anaelezea tukio lilivyotokea.

Tukio la tatu katika kijiji cha Manchali, tarafa ya Chilonwa, Wilayani Chamwino, walimkamata Mazengo Chilatu(28) kwa kosa la kumlawiti mama yake mzazi ambaye hakujulikana jina wala umri wake kwa kumvizia akiwa amelala.

Lingine katika eneo la Maili mbili jijini humo ,ni tukio la Mwanaume mmoja anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 25- 30 ambaye hakufahamika jina lake alifanya matukio matatu ya ubakaji kabla ya kukamatwa na wananchi na kupigwa na wananchi kabla ya kuokolewa na polisi na baadaye kufariki.

Ambapo alifanya matukio hayo kwa watu watatu tofauti kabla ya Julai 4 kukamatwa na wananchi wenye hasira kali na kuupigwa vibaya na kuokolewa na jeshi la polisi hata hivyo alifariki baadaye.

Hata hivyo, amepongeza kazi nzuri inayofanyawa na wanahabari katika kuripoti habari za ukatili huo, ambapo amesema kwa sasa kumekuwa na mwamko mkubwa wa wananchi kuripoti matukio hayo kwa jeshi la polisi.

Hata hivyo Kamanda Muroto amesema matukio ya ukatili mkoani Dodoma yameongezeka kutoka matukio 174 kwa mwaka 2018 na kufikia matukio 517 huku vyanzo vikitajwa kuwa ni ulevi, mmomonyoko wa maadili, uvivu, imani za kishirikina, tamaa na ukatili.