ZANZIBAR: Mwigizaji maarufu wa vichekesho Bongo, Annastazia Exavery ‘Ebitoke’ amesema kazi ya kuuza baa imemfundisha vitu vingi hasa kwenye upande wa maisha.


Akizungumza na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Ebitoke alisema kamwe hawezi kuidharau kazi hiyo wala kuwasema vibaya wanaoifanya kwa sababu anajua changamoto zake na waofanya kazi hiyo siyo kwamba wanapenda. “Ninaheshimu sana kazi ya baa.


Kamwe siwezi kuisema kazi hiyo vibaya kwa namna yoyote ile, najua changamoto zake na wale wanaofanya siyo kwamba wanapenda misukosuko ila ni shida tu,” alisema Ebitoke ambaye ni mmoja wa wasanii wa Bongo Movies walioweka kambi visiwani Zanzibar kwa ajili ya kuifufua tasnia hiyo kupitia Swahiliflix.