KATIBU Mkuu wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali (TAGCO), Bw, Abdul Njaidi, (wapili kushoto), akiwa na Meneja Msaidizi Uhusiano na Itigfaki, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bi. Vicky Msina (watatu kushoto), Meneja Kiongozi Uhusioano na Elimu kwa Umma, Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bi. Lulu Mengele (wane kushoto) na Afisa Uhusiano Mwandamizi kutoka Idara ya Uhusiano na Itifaki BoT. Bw. Lwaga Mwambande (wakwanza kushoto), wakati alipowatembelea kwenye banda la BoT, Mwishoni mwa maonesho hayo Julai 13, 2019.
Bw. Njaidi alizungumza na Afisa Mawasiliano Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bw. Luhende Singu, alipomtembela kwenye banda la NHIF Mwishoni mwa maonesho hayo.
Meneja Kiongozi Uhusioano na Elimu kwa Umma, Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bi. Lulu Mengele (kulia), akizungumza na Bw.Luhende Singu, Afisa Mawasiliano NHIF.
Bw. Njaidi akisalimiana na fisa Mwandamizi wa Masiko na Uhusiano PSPTB, Bi. Shamim Ally Mdee huku Bi. Lulu Mengele akishuhudia.

KATIBU Mkuu wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali (TAGCO), Bw, Abdul Njaidi amewapongeza Maafisa hao kwa kazi nzuri waliyofanya katika kipindi chote cha Maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwenye viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Aliyasema hayo mwishoni mwa maonesho hayo yaliyoanza Juni 28, 2019 na kufikia kilele Julai 13, 2019.

“Kipekee kabisa nimefarijika sana kuona kazi kubwa mliyoifanya ya kutangaza shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi za umma ama kupitia vyombo vya habari au kwa kuwaelimisha wananchi moja kwa moja.” Alisema Bw. Njaidi wakati alipokuwa akiwatembelea maafisa hao kwenye mabanda waliyokuwa wakiyasimamia katika viwanja hivyo maarufu kama Viwanja vya Sabasaba.

Bw. Njaidi ambaye alikuwa amefuatana na Mjumbe wa TAGCO, Bi. Lulu Mengele alisema. “Jukumu letu kubwa ni kuhakikisha wananchi wanapata taarifa muhimu zinazifanywa na Serikali yao kupitia taasisi mbalimbali za Umma na kwa hili nimeliona mimi binafsi wakati nikiwa hapa lakini pia kupitia vyombo mbalimbali vya habari.” Alisisitiza.

Alisema wananchi wanayo haki ya kujua jinsi serikali yao ya awamu ya tano chini ya uongozi wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli inavyowatumikia katika Nyanja mbalimbali kama vile huduma za kijamii zikiwemo, Afya, Elimu, Maji, ujenzi wa miundombinu ambao ndio unaotupeleka kwenye nchi ya uchumi wa kati.

Maonesho ya mwaka huu yalibeba kauli mbiu isemayo “"Usindikaji wa Mazao ya Kilimo kwa Maendeleo Endelevu ya Viwanda.