Oly Ilunga ametaja ukiukaji wa maadili na kuingiliwa kati kazi yake katika barua ya kujiuzulu
Serikali Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imeidhinisha kamati ya kuratibu muitikio wa serikali katika kukabiliana na mlipuko wa Ebola mashariki ma nchi hiyo.

Hatua hiyo imeidhinishwa saa chache baada ya mhusika aliyeongoza jitihada hizo kwa muda wa mwaka uliopita kujiuzulu.

Waziri wa afya Oly Ilunga amejiuzulu katika kulalamikia namna ambavyo mlipuko huo wa Ebola unavyoshughulikia nchini.

Baadhi kutoka ikulu wanaona Dkt Ilunga amejiuzulu kutokana na tuhuma kwamba alikataa kuwashirikisha wengine katika mapambano dhidi ya ugonjw ahuo.

Katika barua yake ya kujiuzulu, Oly Ilunga ameshutumu uamuzi wa rais Félix Tshisekedi kumteua muu mwingine wa kikosi kinachokabiliana na ugonjwa wa Ebola nchini.

Ameshutumu pia alichokitaja kuwa shinikizo la nje la kuidhinihsa chanjo za majaribio kwa ugonjwa huo.

WHO: Mlipuko wa Ebola janga la dharura
Waziri wa fedha Kenya afikishwa mahakamani
Ndege za jeshi la Korea Kusini zaifukuza ndege ya Urusi - Kunani?
Nani kushinda Uwaziri Mkuu wa Uingereza leo?
Mlipuko huo umesababisha vifo vya zaidi ya watu 1,700 katika mwaka uliopita.

Suali kubwa ni kamati hiyo inatarajiwa kuleta tofuati gani katika mapambano dhidi ya Ebola nchini?

Wiki iliyopita shirika la afya duniani (WHO) lilitangaza kwamba mlipuko wa ugonjwa huo kuwa dharura ya afya ya kimataifa.

Janga la ugonjwa wa Ebola liliathiri sehemu kadhaa za Afrika magharibi kuanzia 2014 hadi 2016, na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 11,000.

Kwanini Ilunga anajiuzulu?

Katika barua yake kwa rais Félix Tshisekedi, ameshutumu uamuzi wa kumuondoa yeye kama kiongozi wa kikosi kinachokabiliana na Ebola nchini na badala yake kuchaguliwa kamati ilio "chini ya usimamizi wako binafsi".

Amesema wanakamati hao waliingia kazi yake katika miezi ya hivi karibuni.

Ameshutumu pia "shinikizo kubwa lililopo katika miezi ya hivi karibuni" kutumia chanjo ya majaribio ya Ebola inayopigiwa upatu na mashirika ya misaada na wafadhili.

Amesema chanjo iliopo sasa ndiyo iliothibitishwa kufanyakazi pekee.

Hali ni mbaya kiasi gani Congo?

Mlipuko wa hivi sasa - wa pili kwa ukubwa - ulianza mnamo Agosti mwaka jana na umeathiri majimbo mawili nchin iCongo , Kivu ya kaskazini na jimbo la Ituri.

Zaidi ya watu 2,500 wameathirika na ugonjwa huo huku thuluthi mbili ya idadi hiyo wakiwa wamefariki.