Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema taarifa zilizotolewa na Zitto Kabwe kuhusu mahali alipo Raphael Ongangi raia wa Kenya anayedaiwa kutekwa Juni 24 ni taarifa za mitandaoni na wao hawafanyii kazi mambo ya mitandao.

Hata hivyo Jeshi la Polisi limewataka watu wenye taarifa kuhusu tukio la kutekwa kwa Bw. Ongangi, waziwasilishe ili ziweze kufanyiwa kazi.

Hapo jana  Zitto Kabwe ameelezea simu yake ilivyodukuliwa akihusisha tukio hilo na lile la kudaiwa kutekwa kwa msaidizi wake, Raphel Ongangi raia wa Kenya.

Kutokana na hali hiyo, Zitto amewataka watekaji hao kumwachia huru kwani hana taarifa zake wanazozihitaji. Raia huyo wa Kenya anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana jijini Dar es Salaam, wakati akitoka shuleni kwa watoto wake kwenye kikao cha wazazi.