Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Razaro Mambosasa akizungumza na waandishi habari kuhusiana taarifa mbalimbali ikiwemo ya Mwandishi wa Habari Erick Kabendera. 
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Razaro Mambosasa akimuonesha Askari Feki Daud Ramadhan kwa waandishi habari.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum limesema kuwa Mwandishi wa Erick Kabendera hakutekwa bali Polisi ndio limemkamata kwa mahojiano.

Akizungumza na Waandishi habari Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Razaro Mambosasa amesema kuwa Mwandishi huyo Polisi walimwita akaikadi wito wa Jeshi hilo na kuamua kwenda kumkmata.

Amesema wito wa Polisi kwa Kabendera ilikuwa ni kuhoji uraia wake ambapo kwa mujibu wa Jeshi la Polisi linalomamlaka ya kufanya hivyo na kwenda mbele katika idara ya uhamiaji.

Kamanda Mambosasa amesema kuwa taarifa mbalimbali katika mitandao ya jamii lakini sio Michuzi Blog zilikuwa zikidai kuwa katekwa wakati hakuna ukweli huo.

Wakati huo Jeshi la Polisi limemkamata Askari Feki Daud Ramadhan katika maeneo ya Tabata kwa kujiweka nyota moja ya cheo.

Kamanda Mambosasa amesema Askari Feki huyo alikuwa akifanya njia ya kutapeli watu kwa kutumia sare za Polisi, simu ya mawasiliano ya upepo,pamoja na pingu.Kamanda Mambosasa amesema watampandisha kizimbani kujibu tuhuma hizo.