Katibu mwenezi wa chama cha Demokrasia naMaendeleo Chadema katika kata ya Igurwa Wilayani Karagwe mkoani Kagera amekutwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya katani huku sababu za kujinyonga  zikiwa hazijafahamika.

Akizungumza katika eneo la tukio Diwani wa kata ya Igurwa Bwana WILBAD ABDALA amesema kuwa katibu huyo NURUBET BAKAISHUMBA (35) ambaye pia alikuwa mjumbe katika serikali ya kijiji cha  Bwera amekutwa amejinyonga kwenye mti jilani na nyumba yake.

Amesema kuwa mwili wa marehemu umegunduliwa na baadhi ya wanakijiji july 20 mwaka huu huku akiacha ujumbe wa maandishi unaoeleza kuwa familia yake haihusiki na kifo chake na kumtaka mke wake atunze watoto aliowaacha na kuonesha mali zake zilipo

Bwana Abdala amesema kuwa ujumbe huo aliouacha marehemu amesema kuwa uamuzi huo wa kujinyonga ni wake mwenyewena kwamba wazo hilo alikuwa nalo kwa muda wa mwezi mmoja.

Kwa upande wake katibu wa Chadema Wilaya ya Karagwe bwana AMON MINYANGO amesema kuwa chama hicho kimepoteza mtu muhimu ambaye mchango wake katika maendeleo ya chama hicho ulikuwa mkubwa.