Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza mara baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Burigi Chato Hoteli Park itakayojengwa katika wilaya ya Chato mkoani Geita. Hoteli hiyo itakuwa na hadhi ya nyota tatu na itajengwa na TANAPA na itakuwa na vyumba 50.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza katika hafla ya uzinduzi ya uwekaji jiwe la msingi Ujenzi wa Burigi Chato Hoteli Park.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (kushoto)akiwa baadhi ya Makamishina wa Uhifadhi Kutoka TANAPA na TAWA mara baada ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Rubondo.
Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Burigi Chato Hoteli Park itakayojengwa katika wilaya ya Chato mkoani Geita.
WaHifadhi mpya ya Burigi-Chato inaundwa na mapori ya akiba Burigi,Biharamulo na Kimisi yenye mkubwa wa Kilomita za mraba 4,702 ina wanyama wote maarufu...the big 5 na wingi wa swala kuliko Mbuga yeyote.

Imezungukwa na Lake Victoria,Lake Burigi na River Kagera. Iko mpakani na Rwanda na karibu na Akagera National Park in Rwanda na upande mmoja inapakana na pori la akiba nchini Uganda .Ki ekolojia inafanana na Serengeti.

Kwa sehemu kubwa iko Mkoa wa Kagera yaani iko ndani ya Wilaya za Biharamulo, Muleba, Karagwe na eneo dogo la Chato Mkoani Geita,hence Burigi-Chato National Park