STAA wa Filamu Bongo, Irene Uwoya,  kupitia ukuarasa wake wa Instagram,  amewaomba radhi waandishi wa habari  kwa kitendo chake cha kuwarushia pesa wakiwa katika mkutano wa wanahabari na kusema kuwa hakufanya hivyo kwa lengo la kuwadhalilisha kama ilivyotafsiriwa na  amesisitiza kuwa alifanya kwa moyo mzuri kutokana na juhudi za waandishi wa habari kwenye kusambaza taarifa.


Uwoya alifanya hivyo akiongea na waandishi wa habari waliojitokeza katika ukumbi wa Hyatt Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam jana Julai 15, 2019 kwenye mkutano ulioitishwa na wasanii wa Bongo Muvi ukiwa na lengo la kuzungumzia uzinduzi wa Swahiliflix ambao ni mtandao wa kuuzia muvi, unaotarajiwa kufanyika tarehe 31, mwezi huu mwishoni.

Alichokisema:- Ndugu zangu waandishi wa habari, leo katika press conference ya Swahili Inflix na ndugu zetu waandishi wa habari niliamua kutoa fedha kwa style ya kutunza.

Baadhi yenu mmekwazika kwa kitendo hicho nawaomba radhi sana sikuwa na nia mbaya juu yenu, binafsi nawapenda waandishi wa habari kwani nyie ni watu muhimu sana katika jamii.



Sikufanya hivyo kwa lengo la kuwadhalilisha kama ilivyotafsiriwa.Kama binadamu moyo wangu ulijawa na upendo na furaha iliyopitiliza ndipo niliona niweze kushiriki nanyi furaha hiyo kwa aina ile ya kuwatunza pesa,sababu mara nyingi mmekuwa watu muhimu katika kazi na mambo yote yanayohusu sanaa yetu na jamii kwa ujumla.



Na baadhi ya waandishi ambao kwa bahati mbaya waliharibu vifaa vyao wakati wa kuokota shukrani yangu hiyo(pesa) naomba mniwie radhi na mnisamehe sana na poleni sana kwa changamoto.



Pia kuhusu ndugu zangu waandishi kuwaomba kuvaa suti ile nilikuwa na maana nzuri ya kwamba katika utanashati wenu wa kila siku sisi tulipendelea siku ya tar 31st August katika show yetu inayoandaliwa na Swahili Infilix itakayokuja kuleta mapinduzi makubwa na ukuaji mkubwa zaidi wa filamu zetu za hapa nyumbani tunatamani kuona wote mkiwa katika uniform ambayo itawatambulisha vyema kimavazi ambayo kwa wazo letu tuliweka suti na kiukweli mtapendeza sana na zaidi ya kawaida tulivyozoeana.Nawapenda sana maana hakuna mimi bila nyinyi nathamini na kuwashukuru sana sana.Na zaidi naomba radhi kwa yeyote aliyekwazika kwa namna moja au tofauti.
Asanteni sana.