Nyota wa nyimbo za Bongo Diamond Platinumz hatimaye amezungumza na wanawe miezi minne baada ya kuzuiwa na aliyekuwa mkewe, Zari Hassan, Diamond alikuwa akijaribu kila mbinu kuwatembelea wanawe hata kwa kuzungumza nao ila Zari alimzuia kabisa akidai huwa hajitwiki majukumu ya kuwa baba. 

Kupitia kwenye ujumbe alouchapisha Instagram, Diamond alisema yeye na wanawe walizungumza kwa muda mrefu, jambo lililomfurahisha sana. Diamond hakukosa pia kuchapisha video ya mawasiliano kati yake na wanawe ambapo mwanawe mkubwa Tiffah alionekana kuwa mwingi wa machozi, akidai kumkosa sana babake.


Nillan nawe alionekana kuwa mwingi wa furaha kwani hatimaye alikuwa amemuona babake ambaye alikuwa ameadimika sana. Awali, Zari alidai Diamond alikuwa amewatelekeza wanawe na hangeweza kumruhusu awatembelee wala azungumze nao, madai ambayo Diamond alikanusha vikali.