Aliyekuwa Kiungo wa Klabu ya Simba SC, Haruna Niyonzima, Amekamilisha usajili wake kwa kusaini mkataba wa kuwatumikia mabingwa wa Rwanda Cup, klabu ya AS Kigali inayoshiriki ligi Kuu Nchini kwao.

AS Kigali pia inatarajia kushiriki katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.