MREMBO anayefanya poa kunako anga la Bongo Fleva, Gigy Money amedaiwa kuvishwa pete na mwanaume mwingine tofauti na Mojay ambaye ni mzazi mwenzake, jambo ambalo limeibua gumzo la aina yake. Baada ya picha mbalimbali za mkono unaosemekana ni wa Gigy ukiwa umependeza na pete ya uchumba kusambaa, vijembe vilianza kurushwa kwa Mojay huku wakimwambia alie tu maana kama alidhani hataolewa baada ya kumzalisha basi mwenzake anaolewa.

“Mojay ulie tu maana mwenzako ndio huyo anakwenda kuolewa. Kuzaa na mtu sio ishu, mwenzako anachukua mzigo mazima sasa,” alichangia mbeya moja mtandaoni huku picha hizo za Gigy zikisambaa kwenye kurasa mbalimbali za udaku na kujadiliwa.