Korea Kusini ilisema kuwa ndege ya kijeshi ya Urusia aina ya A-50 ilikiuka anga yake mara mbili
Urusi inasema kuwa imetekeleza doria yake ya kwanza ya pamoja na China , hatua iliyozifanya Korea Kusini na Japan kutuma ndege za kivita angani.

Waziri wa ulinzi nchini Urusi amesema kuwa ndege nne aina ya bombers zikisaidiana na zile za kivita zilipiga doria katika njia ambayo hazikupangiwa kupitia katika maji ya Japan na bahari iliopo mashariki mwa China.

Korea Kusini inasema kuwa ndege zake zilirusha makombora ya kutoa onyo wakati ndege za kijeshi za Urusi zilipoingia katika anga yake. Japan imelalamika kwa Urusi na Korea Kusini kwa tukio hilo.


Kisa hicho kilitokea juu ya visiwa vinavyozozaniwa vya Dokdo/Takeshima ambavyo vinamilikiwa na Korea Kusini lakini Japan pia inadai kuwa vyake.

Korea Kusini inasema kuwa ndege za kijeshi za Urusi na China ziliingia katika anga yake ilio na ulinzi mkali ya KADIZ siku ya Jumanne alfajiri na kwamba ndege moja ya kijeshi ya Urusi aina ya A-50 ilikiuka sheria za kimataifa na kuingia katika anga yake mara mbili karibu na visiwa hivyo. Urusi imekana madai hayo.

Ndege za kijeshi za Urusi na Cjhina aina ya Bombers mara kwa mara zimekuwa zikipitia eneo hilo katika miaka ya hivi karibuni lakini hicho ndio kisa cha kwanza kutokea kati ya Urusi na Korea Kusini.

Wizara ya ulinzi inasema kuwa ndege zake mbili za kijeshi aina ya Tu-95MS zinazobeba makombora zilishirikiana na ndege nyengine mbili za China aina ya Hong-6k katika doria ambayo ilipitia katika njia ambayo hazikupangiwa juu ya anga ya maji yasiomilikiwa na taifa lolote.

Ndege hizo zilisaidiwa na ndege za kijeshi aina ya A-50 pamoja na Kongjing-2000 zinazotumika kutoa onyo .

Luteni jenerali Sergei Kobylash alisema kwamba wakati wa doria hiyo walifukuzwa mara 11 na ndege za kigeni.

Aliwashutumu manohodha wa ndege za Korea kusini kwa kufanya 'hatari' na kundi hilo la angani pamoja na hatari ya usalama wa ndege hizo.

Anasema kwamba ndege hizo za Korea Kusini zilirusha alama za moshi kutoa onyo.