Msanii wa Muziki Bongo wa C.E.O wa lebo ya  Wasafi Classic Baby (WCB), Diamond Platnumz amefunguka kuwa leo watamsaini msaini mwingine kwenye lebo hiyo.

Ikumbukwe msanii wa mwisho kusainiwa na lebo hiyo ni Mbosso ambaye alisainiwa Jan, 27, 2018 ambapo ameweza kutoa nyimbo nyingi na kufanya vizuri.

Hata hivyo bado haijajulikana Diamond Platnumz atamsaini msanii yupi huku mashabiki wakiwa na shauku ya kuongezwa msanii wa kike katika lebo hiyo inayofanya vizuri nchini.

Hadi kufikia sasa lebo ya WCB ina wasanii watano ambao ni Diamond, Harmonize, Rayvanny, Mbosso, Lavalava, Queen Darleen. Pia utakumbuka msanii Rich Mavoko alikuwa kwenye lebo hiyo kutokana kushindwana kibiashara.
Diamond Platnumz kuongeza msanii mwingine kwenye lebo yake ya WCB