Daktari Mbobezi wa Vifo vya Mashaka Atao Ripoti Yake Juu ya Mume Aliemuaa Mkewe
Ni muendelezo wa kesi ya mauaji inayomkabili Godfrey Samweli akidaiwa kumuua mkewe Bahati Husein kwa kumnyonga.

Katika ushahidi uliopita tuliona jinsi gani mtoto wa miaka 10 alivyoieleza Mahakama alivyomshuhudia Godfrey Samweli ambaye ni Baba yake wa Kambo akimnyonga Mama yake Bahati Hussein.

Mtoto huyo anayesoma Darasa la Tatu aliyaeleza hayo mbele ya mbele ya Msajili wa Mahakama, Pamela Mazengo.

Na leo katika ushahidi ni zamu ya Daktari wa Vifo vya Mashaka na Magonjwa mbalimbali kutokea Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dr. Innocent Mosha.

Dr. Mosha ambaye ni mzoefu na mbobezi wa miaka 14 katika sekta hiyo ametoa ushahidi wake akiongozwa na Wakili wa Serikali, Erick Shija.

Katika ushahidi huo, Dr.Mosha ameieleza mahakama kuwa anakumbuka Juni 23/2014 majira ya saa 5 asubuhi alipokea amri ama order kutoka kwa Jeshi la Polisi.

Amri hiyo ikitamtaka kuufanyia Uchunguzi mwili wa marehemu anayeitwa Bahati Hussein.

Dr Mosha amedai kuwa aliomba apatiwe mashahidi wawili kwa ajili ya kuutambua mwili huo wa Bahati Hussein.