Naibu waziri wa kilimo, Hussein Bashe amesema kuwa atajitahidi kadri ya uwezo wake kutimiza  majukumu aliyopewa

Bashe ametoa kauli hiyo leo wakati wa hafla ya kuapishwa kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam, huku akisema Sekta ya kilimo ina changamoto na anaahidi kuzishughulikia.

"Nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kwa yale niliyopewa ili kusukuma gurudumu la maendeleo mbele, Sekta ya kilimo ina changamoto na ninaahidi kuzishughulikia, sitokuangusha na nitatimiza wajibu wangu.

"Mh. Rais nakushukuru kwa imani yako juu yangu na Wananchi wa Nzega, nalifahamu sana suala la Kilimo nafahamu changamoto hizi ambazo zimeajiri 70% ya Watanzania nilizoea kuzisikia tu sasa ntazipata field.

"Sekta ya kilimo tumekuwa tunaita tu kilimo cha kujikimu, ila nafahamu kilimo ni biashara na kilimo ni maisha, uchumi wa nchi hii ambapo ndoto yako ni kujenga uchumi wa viwanda ni lazima wakulima wawe na uwezo na yapaswa tuwatendee haki" -Amesema Bashe.