Mchezaji wa Juventus Cristiano Ronaldo hatakabiliana na shitaka lolote juu ya kutuhumiwa kumbaka mwanadada mmoja mwaka 2009, Las Vegas huko nchini Marekani, wamethibitisha waendesha mashitaka wa Marekani.

Mwanadada Kathryn Mayorga alidai staa huyo alimnyanyasa kingono mwaka 2009 baada ya kukutana Club usiku katika hoteli ya Palms.

Awali ilielezwa kuwa mwaka 2010, mwanadada huyo alikubali kulipwa dola za kimarekani 375,000 (Tsh Milioni 862) na mchezaji huyo ili akae kimya. Mwaka 2018 Mayorga alifungua tena kesi hiyo ya kushutumu kubakwa na mchezaji huyo mwaka 2009.

Taarifa iliyotolewa jana na waendesha mashitaka nchini Marekani inasema kuwa,Cristiano Ronaldo hatakabiliana na shitaka lolote kwa sababu hakuna ushahidi uliopatikana juu ya shutuma hizo za ubakaji.