Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Chege Chigunda, amenyoosha maelezo kuhusu kile kinachoendelea kwa sasa kwenye mitando ya kijamii, kuhusu yeye na msanii mwenzake wa siku nyingi, Mh.Temba.

Akipiga stori na EATV/Radio Digital juu ya taarifa za wawili hao wanatofauti kwa sasa, Chege amesema, “ni mipango tu ya kazi, kuna kufanya ngoma pamoja na kufanya 'collabo', hicho ndio kinachofanya watu waone tuna tofauti lakini hatuna tofauti yotote zaidi ya kubadilisha mfumo wa kazi, ila watu waki-miss tutafanya”.

Pia msanii huyo ameendelea kwa kusema, "hizo ni stori za watu, mimi ninavyoelewa siyo hivyo watu wanavyofikiria na wanavyoongea. Huwezi kumzuia mtu kuongea”.

Taarifa za wasanii hao kutokuwa pamoja zimekuja mara baada ya Chege kufuta picha zote alizowahi kupiga na Mh.Temba kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, na kutoonekana wakiwa pamoja kwa muda mrefu hivi sasa.

Chege na Temba ni wasanii na marafiki wa muda mrefu ambapo walikuwa katika kundi la TMK Wanaume Family lililokuwa na maskani yake Temeke, Dar es Salaam.