Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) kimemteua Rais Dkt. John Magufuli kuwa mgombea wa urais kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu wa 2020.

Image result for mrema
Mwenyekiti wa TLP, Augustino Mrema
Akiongea kuhusu maamuzi hayo, Mwenyekiti wa TLP, Augustino Mrema amesema Halmashauri Kuu ya chama hicho ilifanya uteuzi huo ilipokutana miezi miwili iliyopita ambapo amesema Rais huyo ni bora, tukimpoteza, hatutapata mwingine.

“Tulikutana na Halmashauri kuu ya chama chetu, Kuangalia hali ya upepo wa kisiasa na kuamua kuwa tutasimamisha wabunge na madiwani. Hatuoni sababu ya kusimamisha mgombea Urais mwaka 2020, Kwa mambo anayoyafanya Rais Magufuli, Hatuoni sababu za kushindana naye na kuanza kupoteza Rasilimali. Kwa aliyoyafanya Rais Magufuli, ukitoa Mwl. Nyerere, Kaupeleka uchumi wetu mbele zaidi. Sisi wote tumefanya mambo lakini Rais Magufuli ndiye aliyepaisha uchumi wa Tanzania. Huyu Rais ni muhimu hata kwetu TLP,“Amesema Mrema.

Kwa upande mwingine, Mrema amesema kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 kama CCM wasingemsimamisha Rais Magufuli CCM wangeshindwa kwenye uchaguzi huo.