Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi Iliyoketi jana Jijini Dodoma chini ya Mwenyekiti CCM Taifa Rais Dkt John Magufuli, imemteua Miraji Jumanne MTATURU Kuwa Mgombea Ubunge wa CCM Katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Singida Mashariki baada ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Tundu Lissu kuvuliwa Ubunge.