MTANGAZAJI wa Clouds TV, Casto Dickson ameibuka na kuwavaa aliyekuwa mpenzi wake; Tunda na jamaa wake wa sasa Whozu kuwa waache kumtajataja katika maisha yao mapya waliyoyaanzisha.  Kwenye ukurasa wake, Casto aliwasema Whozu na Tunda kwamba ni watu ambao wanatafuta kiki na kuwaonya wasimhusishe kwenye kiki zao.

“Msitafute kiki zenu kwa majina na jasho la waliotafuta wenzenu kwa jasho lao kwa upuuzi wenu. Kwako wewe X wangu na mpenzi wako tunaweza kutana mahakamani kwa sababu nazijua account zako fake zote! Nimechoka mnaitesa status yangu sio moyo wangu! Utumbo tu huo!” aliandika Casto lakini hata hivyo si Tunda wala Whozu walioibuka kujibu lolote.

Casto na Tunda waliwahi kuwa wapenzi na kapo yao ‘kutrendi’ sana mitandaoni lakini baadaye walimwagana na kila mmoja kuchukua hamsini zake. Sasa Tunda amehamishia majeshi kwa Whozu huku ikielezwa pia penzi lao halina uhalisia bali ni kiki ya wimbo.