Shirikisho la Soka Barani Afrika 'CAf' limemtangaza mwamuzi, Bamlak Tessema Weyesa (39) kutoka Ethiopia kuchezesha mtanange wa fainali ya Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kati ya Senegal  na  Algeria utakaopigwa Julai 19 Mwaka huu.

Katika AFCON ya Mwaka huu, Bamlak Tessema amechezesha mchezo wa Nusu fainali Kati ya Senegal wakishinda dhidi ya Tunisia, Mechi nyingine Ni ya Robo fainali Algeria wakishinda kwa penati dhidi ya Ivory Coast na Mechi za hatua ya Makundi, Ghana wakitoka Suluhu dhidi ya Cameroon, Tunisia na Angola wakitoa Sare.

Fainali hii inazikutanisha timu mbili ambazo zilipangwa katika kundi moja, Algeria na Senegal zote zinatokea kundi 'C' ambapo kulikuwa na timu ya Taifa Stars, Kenya, Senegal na Algeria Kenya na Taifa Stars zote zilitoka hatua ya awali kwenye kundi hilo.